Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, shindano hili limefanyika kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha nafasi ya Qur’ani Tukufu, kuunga mkono madrasa za Qur’ani kama waongoza jamii ya leo, na kama msingi wa elimu na imani katika jamii.
Shindano hili pia liliandaliwa na Wizara ya Wakfu ya Oman kwa lengo la kuwaandaa zaidi washiriki kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya Qur’ani ya ndani ya nchi na ya kimataifa, pamoja na kukuza maadili kama vile ikhlasi.
Taasisi hii inalenga kuwahamasisha vijana wa Kioman kushikamana zaidi na Qur’ani Tukufu kupitia kuhifadhi, kuelewa na kutafakari aya zake, na inajitahidi kuhakikisha kuwa, vijana wanazifanya aya za Qur’ani kuwa kama ubao ulio mbele yao katika maadili na vitendo vyao.
Chanzo: Observer
Maoni yako